Sambaza

Kendrick Lamar Amevunja Rekodi Nyingine Kwenye Hip Hop

October 22, 2012 Kendrick Lamar alibariki masikio ya mamilioni ya mashabiki wa muziki wa Hip Hop duniani baada ya kuachia albamu yake ya kwanza, Good Kid, m.A.A.d city. Albamu hii yenye kolabo na wakali kama Drake na Dr. Dre inatajwa kuwa miongoni mwa albamu bora za Hip Hop za muda wote. Nyimbo kama “Swimming Pools, “Bitch, Don’t Kill My Vibe” na  “Poetic Justice,” zilimpa Kendrick Lamar nguvu ya kutamba kwenye chati tofauti.

 

Ikiwa ni miaka saba imepita, Kendrick Lamar anandika historia ya kuwa rappa wa kwanza kuwa na albamu iliyokaa muda mrefu kwenye chati ya albamu 200 bora(billboard 200). good kid m.A.A.d city imeipiga chini The Emine Show, Albamu ya pili ya Eminem kuuza zaidi ya kopi milioni kumi. Kendrick Lamar na Eminem wote wana historia ya kutolewa na mtu mmoja ambaye ni Dr Dre. Haitakuwa kitu cha ajabu kumuona Eminem anayezeeka huku Kendrick Lamar akiutumia ujana wake kwa kuendeleza kila ambacho Dr. Dre amekianzisha zaidi ya miaka 20.

Imepita miaka miwili tangu Kendrick Lamar alipoachia albamu yake ya nne, D.A.M.N ambayo mwaka 2018 ilimpa tuzo nne za Grammy kupitia nyimbo za Humble na Royalty aliyoshirikiana na Rihanna.

 2,742 total views,  6 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey