Sambaza

Albamu Mpya Ya Kanye West ‘Jesus Is King’, Itachukua Muda Kuwafikia Mashabiki

Albamu mpya ya Kanye West, ‘Jesus Is King’ imeghairishwa kuachiwa kwa mara nyingine tena huku safari hii pakiwa hakuna tarehe iliyotangazwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na TMZ, sababu kubwa ya albamu hiyo kutokuachiwa wikiendi iliyopita kama ambavyo ilitangazwa, ni kutokukamilika baadhi ya hatua za mwisho, Kim Kardashian alitangaza tarehe 27 Septemba kama siku rasmi ambayo albamu hiyo ingeingia sokoni lakini ikasogzwa siku mbili mbele na sasa inaonekana itachukua muda.

Chanzo cha karibu na Kanye kimeiambia TMZ kuwa Kanye anatumia muda mwingi kuisikiliza albamu hiyo, kila anapoisikiliza, kuna kitu anatamani kubadilisha.

Mashabiki wa Kanye West wamekuwa wakiisubiria albamu hii tangu Septemba 2018 kwa mara ya kwanza Kanye alipoitangaza kwa jina la ‘Yandhi’, hata hivyo muda wake ulipofika, Kanye hakuiachia albamu hiyo kwa madai haijakamilika. Jina la albamu limebadilishwa na kuwa ‘Jesus Is King’ (Yesu Ni Mfalme). Kwa mujibu wa walioisikia albamu hiyo yenye nyimbo za dini, Kanye West anadaiwa kuimba maisha yake yaliyopita takribani miaka 15.

 1,889 total views,  6 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey