Sambaza

Kanye West Ameokoka, Hafanyi Muziki Wa Kawaida Tena

Mambo yanaonekana kwenda kikristo zaidi kwa upande wa Kanye West ambaye albamu yake mpya  ‘Jesusu Is King’  yenye nyimbo za dini ilitakiwa kuachiwa Jumapili ya Septemba 29 lakini baada ya kuwasikilizisha bure watu waliohudhuria kwenye ‘sunday servivce’ ya jana, mpaka sasa ni cover pekee yake ambayo imeachiwa huku albamu ikiwa haijulikani itaachiwa muda gani.

Kwa mujibu wa waliohudhuria ‘sunday service’ hiyo, Kanye West ametangaza kuachana na aina ya muziki wake na kuanza kufanya muziki wa dini kwa kile kinachotajwa kuwa amezaliwa upya katika maisha ya Ukristo..

Moja ya kitu kinachoifanya Jesus Is King kusubiriwa kwa hamu zaidi, ni muunganiko wake na ‘Jesus Is King’ (Kanye West Experience) documentary ambayo ni maisha halisi ya Kanye West katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Mwaka mmoja kabla ya kutangaza ujio wa ‘Jesus Is King’, Kanye alitangaza angeachia ‘Yandhi’, Albamu ambayo ilighairishwa kwa kile ambacho Kanye alisema atatangaza tarehe ya kuiachia atakapokuwa ameikamilisha. Jesus Is King inasemekana kuwa ni YANDHI imebadilishwa jina na baadhi ya nyimbo zilizokuwa ndani yake.

Endelea kufuatilia Global Radio kwa taarifa zaidi kuhusu albamu hiyo na stori nyingine za burudani.

 3,441 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey