Traviss Scott Atangaza Ujio Mpya Baada Ya AstroWorld
Agosti 28 mwaka huu aliiachia Look Mom I Can Fly, Dokyumentali yake ambayo ndiyo projekti yake mpya baada ya albamu yake ‘AstroWorld’ ya mwaka 2018. Mwaka huu ameshiriki kwenye albamu mpya ya Post Malone, Hollywwod’s bleeding kwenye wimbo unaoitwa ‘Take What You Want‘. Travis Scott ametangaza kuwa anaachia wimbo mpya wiki hii unaoitwa “Highest in the Room.” Utaachiwa rasmi Ijumaa, Oktoba 4.
HIGHEST IN THE ROOM 10/4https://t.co/AJ4e7OI3tq pic.twitter.com/k2ETrAt1lD
— TRAVIS SCOTT (@trvisXX) September 30, 2019
Mapema mwaka huu, Travis Scott ambaye jina lake halisi ni Jacquees Webster, alishiriki kwenye albamu ya ‘Game Of Thrones‘, pia aliungana na mwandada SZA kwenye wimbo ‘Power Is Power‘ wa The Weeknd. CHopstix ni wimbo unaopatikana kwenye albamu CrasH Talk ya Schoolboy Q ambao pia ni miongoni mwa kazi alizofanya Traviss Scott mwaka huu.
1,850 total views, 3 views today