Eddie Murphy Anajutia Kupoteza Muda Kwenye Utani
Muigizaji wa Mmarekani ambaye ni mchekeshaji maarufu, Eddie Murphy amesema anajutia alivyopoteza muda wake kwa kufanya vichekesho vilivyokuwa havisaidii kubadilisha jamii, badala yake alitaka kufanya kwa ajili ya kujitimizia mahitaji ya moyo wake,
Eddie Murphy ambaye yupo kwenye hatua za mwisho ili kukamilisha ujio wa filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina Dolemite Is My Name, pamoja na dili la utangazaji wa kipindi cha Saturday Night Live, amesema alikuwa mvulana mdogo ailiyekuwa akijaribu bahati yake, lakini alikuwa kama mjinga kwani alifanya mambo mengi ya kufurahisha lakini yalikuwa hayafundishi.
Eddie Murphy Ameyasema hayo alipofanya mahojiano na New York Times ambapo alizungumzia mambo mengi, pointi kubwa ikiwa ni jinsi miaka zaidi ya thelathini ya uchekeshaji ilivyombadilisha.
Eddie Murphy aliiambia NYT kitu anachoweza kujielezea kwa sasa ni mtu tofauti ambaye haishi kama mwanzo, mkali huyo wa Coming To America, amesema anajisikia vibaya akikumbuka utani alioufanya enzi za ujana wake kuhusu mambo yaliyokuwa na manufaa kwenye jamii. Ameahidi kuja na utani utakaokuwa na ushawishi pamoja na kupinga ubaguzi.
Maamuzi ya EddieMurphy kuja na stand up comedy ya kufundisha yalitokana na maongezi kati yake na Andy Cohen pamoja Titus Burgess, waigizaji wenzake walioshirikiana nae kupata mawazo ya kuiendeleza na wamecheza pamoja filamu hiyo ya Dolemite Is My Name.
Dolemite Is My Name ni filamu ya vichekesho iliyochezwa Marekani mwaka 2019 , Eddie Murphy amecheza kama Muandaaji wa muvi anayeitwa Rudy Ray Moore, filamu inaanzia mwaka 1975 ikiwa na stori ya mtu anaitwa Dolemite. Kwa mara ya kwanza filamu hiyo ilionekana Septemba 7,2019, na itaachiwa kwa muda Oktoba 4,2019 kabla ya kuachiwa rasmi na NetFlix Oktoba 25,2019.
2,208 total views, 3 views today