Sambaza

Jeezy Anastaafu Muziki Na Kuhamia Kwenye Michezo

Tangu alipoiachia albamu yake TM104 aliyoitangaza kuwa ya mwisho, inawezekana huu ndio utakuwa mwisho wa muziki wa Rappa huyu mwenye asili ya Atlanta Marekani, Jeezy ameamua kustaafu muziki ili aendeshe kampuni yake ya michezo ambayo ameitangaza kwenye siku yake ya kuzaliwa (Septemba 28).

Wakati wa kuitambulisha kampuni hiyo, Jeezy alisema lengo lake kubwa ni kusaidia wenye vipaji vya michezo watimize ndoto zao na kuishi maisha waliyoyatamani.

Japo hakuna taarifa rasmi zilizothibitisha ni lini kampuni hiyo itaanza kufanya kazi, vyanzo vinadai kampuni hiyo itakuwa ikihusika na wachezaji wote wa NFL na NBA.

Jeezy sio mwanamuziki wa kwanza kuwekeza kwenye michezo, wafanyabiashara wakali kama Jay-Z na Lil Wayne wamekuwa wakifanya biashara hiyi kwa miaka kadhaa, na pengine watakuwa wanahusika kwa namna moja katika kumshawishi Jeezy kuanzisha kampuni yake inayoitwa  Sport99.

 

 2,235 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey