Sambaza

Post Malone Anavyowakimbiza Billboard

Hakuna cha kumzuia Post Malone. Albamu yake mpya Hollwood’s Bleeding inaongoza nafasi ya kwanza kwenye chati ya albamu 200 za billboard kwa wiki ya tatu mfululizo.

Billboard wamesema Hollywood’s Bleeding imefikisha units 149,000 wiki iliyoisha sept 26. Pia kwa mwaka huu nia albamu pekee iliyokaa kwenye nafasi hiyo kwa wiki tatu. Ni albamu ya kwanza kufanikiwa kufika hatua hiyo tangu kolabo ya Lady Gaga na Bradley Cooper, Star is Born effort.

Albamu nyingine zilizofanikiwa kukaribia rekodi hiyo mwaka huu ni, Hoodie SZN ya A Boogie Wit da Hoodie na When We All Fall Asleep, Where Do We Go? ya Billie Elish.

Albamu ya Post inafuatiwa na The Owl ya Zac Brown Band kwenye nafasi ya pili na Nine from Blink ya 182 namba 3. Taylor Swift Lover ipo nafasi ya 4 huku nafasi ya tano ikishikwa na So Much Fun ya Young Thug ambayo ni albamu yapili kwenye albamu 5 bora wiki hii.

 2,296 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey