Rasmi Gigy Money Anatambuliwa Na BASATA
Kuanzia sasa Giggy Money ni mwanamuziki anayetambulika rasmi na Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA).
Tangu mwaka 2017, Gigy Money amekuwa akijitahidi kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wake bila kuchoka, Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Gigy Money alikuwa akifanya kazi ya kufurahisha mashabiki wakati mamlaka zenye dhamana ya kazi yake hazimtambui.
Leo (Oktoba 1) kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy ameweka post zinazomuonyesha akipokea vielelezo vya uhalali wa kazi yake kutoka kwa Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza .
“Mapema Leo nimeweza kupata bahati yakujisajili katika baraza la Sanaa la Taifa letu pichani nikiwa Na Mh mungereza ? wa BASATA“. ameandika Giggy.
3,957 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa