Sambaza

Baada Ya Harmonize Sasa Ni Rayvanny Kupokea Tuzo Hii

Februari 7, Rayvanny aliichia ‘Tetema’ ambayo ni kolabo yake ya tano na supastaa Diamond Platnumz, Tetema ndiyo video ya Rayvanny yenye mafanikio makubwa kwenye mtandao wa YouTube. Ikiwa na miezi saba tangu iachiwe, Video ya tetema imetazamwa zaidi ya mara milioni 30.

Wakati akifurahia kufikisha watazanaji zaidi ya milioni 30 wa video hiyo, Rayvanny anaunganisha furaha yake kwa kuonyesha tuzo aliyoipokea kutoka makao makuu ya YouTube California Marekani. Muimbaji huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha tuzo hiyo aliyopewa baada ya kufikisha ‘Subscribers Milioni moja’ kwenye YouTube Chanel yake ambayo ina watazamaji zaidi ya milioni 197.

Kwenye video aliyoposti Instagram, Rayvanny amemshukuru Mungu, menejimenti yake na mwisho kabisa ni mashabiki wake ambao wanahusika kwa asilimia nyingi kwenye upatikanaji wa tuzo hiyo ya Dhahabu. Pia Rayvanny ameahidi kuachia wimbo mpya siku za hivi karibuni.

View this post on Instagram

1M Subscribers ??? ??? @youtube

A post shared by VANNYBOY (@rayvanny) on

Rayvanny anaungana na Yemi Alade, Davido, na Harmonize kama wasanii wa Afrika waliopata tuzo hii kwa kufikisha subscribers zaidi ya milioni moja huku Diamond Platnumz akiwa kinara kwa zaidi ya subcribers milioni 2.

 3,652 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey