Sambaza

Harmonize Amelamba Shavu La Madini Ya Tanzanite

BAHATI inamnyookea! Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ Harmonize amepata shavu la kutangaza madini ya Tanzanite.


Akizungumza na gazeti la #RisasiMchanganyiko, Balozi wa Tanzanite nchini, Nangasu Warema alisema kwamba Harmonize atakuwa akiyatangaza madini hayo ndani na nje ya nchi kupitia muziki wake. “Tumeshaongea na Harmonize na ameahidi kuanza kuyatangaza madini haya ya Tanzanite, hivyo nawaomba Watanzania wote waanze kujisikia fahari na madini haya kwani ni yetu sote,” alisema Warema.


Warema alitoa rai kwa Watanzania kujivunia rasilimali zilizopo nchini kwani Tanzanite ni madini ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee duniani. “Kikubwa ni kupenda vya kwetu, itakuwa jambo jema kama Watanzania wataanza kuvaa madini haya kama wanavyovaa vitu vya madini mengine.

 4,831 total views,  6 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey