Sambaza

Kylie Jenner Na Travis Scott Wameachana

Inadaiwa wawili hao hawajaonekana pamoja muda mrefu tangu walipoonekana mara ya mwisho kwenye red carpet ya uzinduzi wa dokyumentali ya Travis Scott, Look Mom I Can Fly. Wiki moja baada ya uzinduzi huo, Kylie na Traviss walipata nafasi ya kuuza sura kwenye jarida la Playboy ambapo walizungungumzia maisha ya mapenzi, malezi ya mtoto wao na muunganiko wao,

Kwenye issue ya Playboy, Kylie Jenner alisema yeye na Traviss wanafanana mitazamo na vitu wanavyovipenda, tofauti na muunganiko wao mzuri, Kylie alidai kama Traviss ni zaidi ya rafiki kwake, licha ya changamoto wanazokutana nazo lakini wamechagua kuwa imara.

Chanzo cha karibu na Kylie Jenner kimevujisha stori ya wawili hao kuuvunja uhusiano wao uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili, “kila mmoja yupo single, sasa hivi wanashirikiana kumlea mtoto wao Stormi waliyempata mwanzoni mwa 2018”. chanzo hicho kimeiambia TMZ.

Inasemekana hii sio mara ya kwanza kwa wawili hawa kuchukua breki kwenye mahusiano yao. Mapema mwanzoni mwa mwaka 2019 ziliibuka tetesi za wawili hao kumwagana kwa kile kilichodaiwa ni Kylie kumtuhumu Travis kwa kumsaliti na mwanawake mwingine.

 

 4,181 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey