Sambaza

OfficialLynn Ametangaza Mabadiliko Makubwa Kwenye Muziki Wake

Mwanamuziki Lynn ambaye amewahi kuwa video queen (vixen),Leo Oktoba 2, amemtumia Diamond salaam za bethidei huku akimshukuru kwa kila alichomfanyia ikiwa ni pamoja na kuhusisha kile alichokisema ni mahusiano yao ambayo yaliibuka baada ya wawili hao kufanya kazi kwa ukaribu. Lynn ambaye alianza kung’aa kupitia video ya wimbo ‘Kwetu’ wa Rayvanny, amemshukuru Diamond Platnumz na timu nzima ya WCB kwa mchango wao kwani amejulikana zaidi, hasa alipoanzisha mahusiano na Diamond.

Lynn ameyasema hayo kwenye kipindi cha Bongo255 alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya ‘Pepea’,  Kwenye interview na Stewart George pamoja na Rashid Mbegani, Lynn amefunguka mengi ikiwemo kuandikiwa nyimbo zake zote, kitu ambacho haoni aibu kukisema. Lynn amekubali kusema ndiyo kwenye swali lililouliza kuhusu uhalali wa muziki wake kwa kuthibitisha umaarufu aliokuwa nao umemrahishia kupata mapokezi mazuri kwenye muziki.

“Kutokea kwenye vixen imenisaidia kufanya muziki kwa urahisi, nimepata nafasi ya kujitambulisha kama mimi ni mwanamuziki” allisema Lynn ambaye alishikwa na kigugumizi kujibu baadhi ya maswali kama maana ya wimbo wake wa chomeka pamoja na tafsri ya neno brand licha ya kusema anajibrand.

Lynn amesema kwa sasa muziki bado haujaanza kumlipa japo anaamini kuja kuwa mmoja kati ya wanamuziki wakubwa wanaolipwa vizuri, hivyo anaendelea kufanya kazi na mashabiki wake wategemee mabadiliko mengi makubwa kutoka kwake.

Lynn Kwa sasa anatamba na wimbo wa Pepea aliomshrikisha muimbaji wa taarab, Prince Amigo.

 

“Kwasasa muziki haujaanza kunilipa lakini naamini mafanikio yatakuja, Lynn alipoulizwa kuhusu  Winnie aliyeimba Ado na Marioo amesema hamjui labda akisikia wimbo huo ndipo atamjua.
Wimbo wake ‘Chafu’ ambao umeandikwa na Marioo, video yake imefanyika Afrika kusini lakini Marioo hakuonekana kwenye video hiyo, mrembo Lynn ameweka sawa ishu hiyo kwa kusema “Marioo hakukataa kufanya video na mimi, nilikuwa tayari kumlipia kila kitu South Africa, lakini kuna vitu kwa upande wake havikukamilika akashindwa kusafiri.”.

Lynn amewataka wanaomuonea wivu kwenye starehe anazofanya waache kumsema vibaya kuhusu maisha yake kwani anajua anachokifanya kama ni kuhusu biashara anafikiria muda wa kutambulisha bidhaa yake haujafika.
Lyn amepata kigugumizi kujibu anatumiaje umaarufu wake kupata mikwanja, “mimi…. unajua ahm ….nautumia vizuri mimi ni mtu fulani tofauti na wasanii wengine hata ukiangalia instagram tuna utofauti kwasababu napata madili ambayo unaelewa wengine hawajawahi kupata,”

Kwenye eneo hili ifike pointi muziki upewe heshima yake, wasanii wanahitaji kuwa na wasemaji wao, Lynn ana mawazo ambayo akisikilizwa yanaweza kuwa biashara, nilichojifunza anashindwa kuelezea vitu vya msingi sana ikiwemo utofauti wake na wasanii wenzake. Kama angekuwepo mtu anayeifahamu vizuri biashara yake na kumfahamu kama Irene ambaye angesimama kama manager na msemaji wa binti huyu mwenye miaka 20, biashara yake ingeweza kukua kwa haraka.

Lynn ana mapungufu kwenye muziki, watu wanaomzunguka wanapaswa kumshauri na kumpa akili ya kucheza na upepo wa Media kabla kijiti hakijaondoka mkononi kwake na kudondokea mikononi mwa mrembo mwingine anayejua kuimba na mwenye timu makini ambaye anaweza kuja na aina ya muziki wa Lynn akaufanya kiprofesheni na akawa habari kubwa.

 3,390 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey