Sambaza

Prince Harry Na Mkewe Meghan Kwenye Miradi Ya Ajira Afrika

Baada ya siku sita za kutengana kila mmoja akiwa na ziara yake nchini Afrika kusini, hatimaye Prince Harry na mkewe Meghan wamekutana Johanesburg Afrika Kusini, kuendeleza siku kumi za ziara yao ambapo wamejifunza mambo mengi kuhusu vijana wasiokuwa na ajira.

Prince Harry na Meghan wamejifunza jinsi taasisi ya Youth Employment Service (Yes) inavyotengeneza mamilioni ya fursa za ajira kwa vijana, taasisi hiyo ambayo ilizinduliwa April 2018 na Rais Cyril Ramaphosa, inatarajiwa kuanza kufanya kazi baada ya miaka mitatu.

Katika kituo cha Aquaponics, mjasiriamali mchanga aliwaambia Meghana na Harry jinsi kituo hicho kilivyotoa fursa katika jamii yake, kusaidia eneo linalozunguka migahawa na maduka makubwa kwa usambazaji wa mazao safi yanayopatikana nchini humo.

Wanandoa hao walitembelea Blossom Care Solutions, kuwasikiliza wasichana 14 wadogo ambao wamekuwa wakipewa mafunzo kabla ya kukabidhiwa majukumu kwenye uandaaji wa taulo 80,000 za kike kila mwezi. Ikiwa ni siku yao ya tisa Afrika, wawili hao wameangazia mambo kadhaa wanayoyapenda ikiwemo kuwanyanyua wanawake.

Kwenye siku yao ya mwisho Johanesburg, wanategemea kukutana na Graca Machel, mjane wa Nelson Mandela. Ziara ya wanandoa hao ambao ni familia ya malikia wa Uingereza, inatarajiwa kufikia mwisho wiki hii ambapo wawili hao watakutana na Rais Ramaphosa na mke wake Dr. Tshepo Motsepe.

 3,831 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey