Sambaza

Kylie Jenner Amemuacha Travis Scott Kwa Sababu Ya Kuongeza Familia

Jumatano (Oktoba 2), chanzo cha karibu na Kylie Jenner kilizivujisha taarifa za model huyo kuachana na Travis Scott ambaye ni baba wa mtoto wake Stormi Webster.


Kwa mujibu wa chanzo hicho,kuna mambo mengi yaliyosababisha wawili hao kuachana, lakini kubwa zaidi ni Travis Scott kukataa kuongeza mtoto wa pili.
Travis Scott ambaye Oktoba 4 ataachia kolabo yake na LilBaby, amekuwa akipinga wazo la kuongeza familia huku akitaka kila mmoja wao kuwekeza muda kwenye biashara yake.


Kylie Jenner anaripotiwa kutomuamini mpenzi wake, hivyo amekuwa akimuwekea vikwazo vingi kwa kutaka kufanyiwa kila anachotaka. Inasemekana Kylie anajifunza mambo mengi kupitia dada yake Kim Kardashian ambaye ana watoto wanne na Rappa Kanye West waliyedumu kwenye ndoa kwa miaka 6.
Hata hivyo Kylie na Travis bado hawajajitokeza na kuielezea ishu hiyo hadharani.

 3,664 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey