Dogo Janja Aahidi Kumfurahisha Marehemu Ruge
Jumamosi (Oktoba 5), tamasha la Fiesta litaacha burudani kwa wakazi wa mkoa wa Kagera na maeneo yake ya jirani, Dogo Janja akiwa ni miongoni mwa wanamuziki watakaoburudisha usiku wa kesho. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameposti picha akiwa na mama mzazi wa muasisi wa tamasha hilo marehemu Ruge Mutahaba.
Kwenye picha hiyo Dogo Janja ameandika maongezi yake na Mama yake Ruge yalivyokuwa, mwanamuziki huyo mwenye asili ya Ngarenaro, ameonyesha kumkumbuka marehemu na kuahidi show ya kumfurahisha.
“Nilipotua tu kwenye ardhi ya bukoba…fikra zangu moja kwa moja zikaniambia kwamba ntakutana na RUGE JASIRI MUONGOZA NJIA!! Coz nakumbuka mara ya mwisho tulimleta hapa na hatukurudi nae.. natoka nje tu nakutana na mamaake JASIRI MUONGOZA NJIA bila kumuuliza kitu akanijuza kua kakako bado kalala pale pale mlipomuwacha.. nikamjibu Mwanga wa bwana uendelee kumuangazia ntaimba mpaka ajue leo nipo BUKOBA na atafurahia show yangu” ameandika Dogo Janja kwenye picha hiyo iliyopigwa uwanja wa ndege wa Bukoba, Dogo Janja ameahidi kufanya show ambayo itamfurahisha marehemu aliyelala mahali walipomuacha mara ya mwisho.
#RIPRugeMutahaba.
3,167 total views, 3 views today