Sambaza

Kifo Cha Mac Miller; Watatu Wanashikiliwa Kwa Kumuuzia Madawa Ya Kulevya

Wanaume watatu wamekamatwa kwa kosa la kumuuzia Mac Miller madawa yaliyosababisha kifo chake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano jioni (Oktoba 2), Cameron James Petiti, Stepehen Walter na Ryan Reavis wote wamekamatwa kwa kosa la kumuuzia Mac Miller madawa ya kulevya aina ya Cocaine na vidonge vya Oxycodeone.

Watatu hao wamekuwa na historia za kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kesi tofauti za madawa ya kulevya, lakini sasa wote wanashikiliwa kwa kosa moja linalomuhusu Mac Miller ambaye aliripotiwa kufariki dunia Septemba 7, 2018 kwa kile kilichodaiwa ni matumizi yaliyozidi kiasi(Overdose) ya madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa, hukumu ya watu hawa inaweza kuwa miaka 20 jela kwa kosa la kusambaza madwa ya kulevya, na iwapo watapatikana na hatia ya kusababisha kifo cha Rappa huyo, wanaweza kufungwa maisha bila msamaha.

Rest In Peace Mac Miller.

 3,504 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey