Sambaza

Alikiba Amesikia Kilio Cha Mashabiki Wake, Huu Ni Ujio Mpya?

April 26, 2019, Alikiba aliachia ‘Mbio’ ambao ni wimbo wa peke yake wa mwisho, miezi takribani mitano imepita King Kiba bado anaendelea kuishi style yake ya ukimya wa muda mrefu, licha ya kuwa amesikika kwenye kolabo kadhaa ikiwemo ‘bembea’ na Aslay ambayo ni miongoni mwa nyimbo zinazopendwa wakati huu.

Wakati ambao mashabiki wa msanii huyu wanatamani kusikia muziki wake mpya, Alikiba yupo na harakati nyingine nyingi kikubwa anachoonekana kukitumia kwa muda mwingi ni charity.

Kama unafuatilia ukurasa wa Instagram wa @Officialalikiba, utagundua kwenye Bio yake hakuna link inayoonyesha project yoyote, sio yake wala Kings Music au Bembea aliyoshirikishwa na Aslay, Hii inamaanisha sehemu ya website haijajazwa, tena makusudi kwani Alikiba sio msanii wa kuacha kupromote link zake kwenye akaunti yake yenye zaidi ya followers milioni 4.

Wakati unaangalia Bio yake kwa ukaribu, Cheki picha za Alikiba vizuri, utaona post zake zote zinamaanisha vitu, Post iliyofanya tuandike hapa ni picha ambayo Alikiba ameiweka mtandaoni humo Jumamosi asubuhi (Oktoba 5). Boss huyo wa Kings Music amepost picha ikimuonyesha amesimama pembeni ya gari la starehe huku amevalia IVY Cap na koti la heshima, Alikiba anaonekana kuwa kwenye mazungumzo ya muhimu na mtu ambaye hatujapata nafasi ya kumjua kutokana na mkao wake wa kumtega mgongo mpiga picha.

View this post on Instagram

? #kingkiba

A post shared by alikiba (@officialalikiba) on

Baada ya kuiangalia picha hii kwa muda mrefu utagundua haina caption zaidi ya #KingKiba, tulijaribu kufikiria utofauti wake na picha nyingine ambazo Alikiba amepost. Hii inatuonyesha kama ni kwenye set ya video, ni wazi kama Alikiba amesikia kilio cha mashabiki wake na huenda huu ukawa ni ujio wa video ya wimbo mpya baada ya Mbio.

 5,876 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey