Ameishitaki iPhone Kwa Sababu Ya Mapenzi Ya Jinsia Moja
Mwanaume mmoja wa Urusi amewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya kampuni ya Apple, akidai kuwa programu ya iPhone ilimgeuza kuwa mtu anayeshiriki mapenzi wa jinsia moja. Ameyasema hayo baada ya tukio jingine linalohusisha programu ya malipo ya ya kimtandao ya GayCoin yanayohusishwa na wapenzi wa jinsia moja.
Anasema alipata madhara sana ya kihisia na anadai alipwe Shilingi milioni 34,053,752 kwa mujibu wa nakala ya mashtaka iliyolifikia shirika la habari la AFP.
Wakili wake , Sapizhat Gusnieva, anasema kuwa mteja wake “ana hofu kubwa, na anaumia “, na kuongeza kuwa kesi yake iliyowasilishwa mjini Moscow ni ya “uhakika”. Katika mashtaka yaliyowasilishwa tarehe 20 Septemba, inadaiwa malipo ya biashara za mtandaoni yanayohusishwa na wapenzi wa jinsia moja “GayCoin” yalilipwa kupitia programu ya smartphone, kinyume na mfumo wa Bitcoin aliokuwa ameutumia kuagiza bidhaa.
Malipo ya Crypto-currency hutumia pesa – ni aina ya pesa zinazotumiwa kwa ajili ya mtandao- na Bitcoin na GayCoin ni baadhi ya pesa za aina hiyo. Kwa mujibu wa mlalamikaji pesa za GayCoin crypto-currency zilimfikia zikiwa na ujumbe unaosema : “Usihukumu bila kujaribu”.
” Nilifikiria, kiukwelii , ni kwanini nihukumu kitu bila kukijaribu ? Niliamua kujaribu mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja, sasa nina mpenzi wa kiume na sasa sijui jinsi ya kuwaelezea hili wazazi wangu.” ,” uliandikwa waraka wa mashtaka ya Mrusi huyo.
Mwaka 2013, Urusi ilianzisha sheria dhidi ya ” uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja”, ambayo inapiga marufuku rasmi “kueneza mitindo ya maisha ambayo ni kinyume na maisha ya kawaida kwa watoto na vijana wadogo ” .
Mahakama itamsikiliza mlalamikaji tarehe 17 Octoba, Apple bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na shutuma hizo dhidi yake.
2,243 total views, 3 views today