Sambaza

Angelina Jolie Amesimulia Mabadiliko Baada Ya Kuachana Na Brad Pitt

Angelina Jolie amefanya intavyuu kadhaa ambapo ameongea kuhusu umama, watoto wake na mume wake wa zamani Brad Pitt waliyetengana mwaka 2016.

Kuhusu kuachana na Brad Pitt, Angelina Jolie amesema alikuwa amepotea na wakati huu anahisi kurudi kwenye hali yake ya kawaida kwani kitendo cha kuachana na Baba watoto wake kilimuumiza.

“Ilikuwa ngumu, Niliumia sana, niliumia sana, niliumia. Kwa upande mwingine, ilikuwa hali ya kuvutia kugundua unyenyekevu niliokuwa nao nilionekana kutokuwa na maana. Mwishowe nikasema huyu ni binadamu. Pamoja na yote, nilikuwa nikishughulikia maswala kadhaa ya kiafya. Vitu hivi vyote vimenituliza na kunikumbusha jinsi nilivyo na bahati ya kuwa hai. Ni funzo ninalopitia kwa watoto wangu: kwani ndio kila kitu kwangu,ninaangalia uwezekano wa kutafuta furaha kila siku kabla ya kuabudu vitu vingine. alisema Angelina Jolie.

Wawili hawa walifunga ndoa mwaka 2014 na kuachana mwaka 2016, Angelina na Brad walifanikiwa kupata watoto watatu wa kuzaa wenyewe na watatu waliasiri kutokea nchi tofauti. Watoto wote walibaki chini ya malezi ya mama yao.

 2,763 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey