Sambaza

Fabolous Amewakutanisha Davido Na Jeremih Kwenye Choosy

Agosti 10, 2018, Fabolous aliachia wimbo wake ‘Ooh Yea’ ambao alimshirikisha Ty Dolla $ign, Baada ya ukimya wa mwaka mzima Fabolous amerudi na wimbo mpya ‘CHOOSY’ kwa ushirikiano wa Jeremih na Nigerian supastaa Davido.

Wimbo huo mpya umeandaliwa  na Hitmaka na Swiff D, umetengenezwa kwa muziki wa gitaa na mdundo wa afrobeats ambao ukiusikiliza vizuri unaweza kuhisi kuna ‘Unforgetable’ ya French Montanna.

Jeremih ameanza na neno ”Choose” kwenye korasi ya wimbo huo, akiwa na maana ya  ”Choosy” kama jina la wimbo linavyosomeka , Fabolous amezikamilisha verse zake mbili huku Davido akijitokeza dakika za mwisho kabisa akitumia kionjo cha wimbo wake ‘If”’

Video ya ‘Choosy’ imefanyika kwenye nchi ya Cape Verde. Imetengenezwa kwa umakini sana, rangi na shot ni vitu timu ya production ilikuwa imezingatia sana.

Gerald Victor ndiye muongozaji (Director) wa video hiyo.

 

 1,848 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey