Sambaza

Moni Centrozone Alivyotumia Moyo Wa Vanessa Kuinogesha La Moto

Imepita miezi miwili tangu Vanessa Mdee alipouachia ‘Moyo’ kama wimbo wa kwanza kutokea kwenye Expensive, EP ambayo The Original Cash Madame anajipanga kuiachia mwaka huu. Moyo ni wimbo ambao umemuunganisha Vanessa na wasichana/wanawake wengi ambao wamekuwa wakipitia mambo magumu kwenye mahusiano yao ya kimapenzi.

Ujio wa ‘Moyo’ ulikuja sambamba na taarifa za Vanessa Mdee kuachana na Bongofleva supastaa African Boy JUX aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu. Vanessa Mdee aliutumia wimbo huo kuulaumu na kuhukumu moyo wake kwa kumkutanisha na watu wanaoishia kumuumiza kitu ambacho moja kwa moja tunakihusisha na kuachana kwake na Jux, Moni Centrezone amekitumia kama kionjo ambacho kimependezesha wimbo wake mpya ‘La Moto’ alliouachia Agosti 22, Kwenye wimbo wake Moni anasikika akiimba’Mabrotherman hawako loyal, wamemfanya Vanessa akaua moyo‘.

Video ya ‘La Moto’ imeachiwa Alhamisi  (Oktoba 1), Video hiyo yenye urefu wa dakika 3;50 imeongozwa na Nicklass kwa ubunifu wa hali ya juu. Imekuwa kitu cha kawaida kwenye video za nyimbo kama hizi kuonekana muimbaji akiwa na rafiki zake, video vixen na watu wengine wa ziada lakini wakati huu Moni amefanya kitu tofauti kidogo, kwenye video hii ameonekana yeye na mrembo wake pekee.

 

 3,276 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey