Ombi La R. Kelly Kutibiwa Limekataliwa, Kesi Yake Mpaka 2020
Wiki iliyopita tuliandika ishu ya mwanasheria wa R. Kelly kuwasilisha mahakamani ombi la mteja wake kutolewa jela ili akatibiwe. Taarifa tuzlizozipata zinadai jaji anayesimamia kesi ya muimbaji huyo, amekataa ombi la kumtoa.
Kwa mujibu wa timu yake, R.Kelly ana matatizo ya afya ikiwemo kupata ganzi mikononi, wasiwasi na hernia isiyotibika, hivyo anatakiwa kuwa nje ya jela kwa ajili ya matibabu lakini hata hivyo upande wa serikali unadaiwa kutochukua hatua yoyote.
R. Kelly ataendelea kusota jela mpaka Aprili 27, 2020 ambapo kesi yake itasikilizwa tena. Mwanamuziki huyo anashitakiwa kwa kosa la kuwanyima watoto haki zao kwa kuwatumikisha kingono.
2,375 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa