Sambaza

Travis Scott Amevunja Ukimya Tetesi Za Kuachana Na Kylie Jenner

Travis Scott amevunja ukimya wake kufuatia tetesi za kuachana na Kylie Jenner,ambaye ni mama wa mtoto wake wa kike Stormi Webster.

Rappa huyo mwenye umri wa miaka 28 amezungumzia jinsi stori za yeye kumsaliti mpenzi wake zinavyomuathiri. Travis amekuwa akituhumiwa kutoka kimapenzi na msichana anayeitwa Rojean Kar, hii imetumika kama moja ya sababu za kuachana na bilionea huyo mdogo mwenye umri wa miaka 22.

Travis amekanusha uvumi huo kupitia Instagram story, ambapo ameongea kwa mara ya kwanza tangu zisikike taarifa za kufikia mwisho wa mahusiano yake na Kylie.

“Inaathiri sana wakati unaona mambo ya uongo yakisemwa juu yako, tena hadithi hizi za mimi kumsaliti mpenzi wangu sio kweli, ukweli ninaoujua mimi naweka muda wangu kwa ajili ya familia, maisha na muziki”

Travis Scott na Kylie wamekuwa kwenye mahusiano ya mapenzi tangu mwaka 2017 na kufanikiwa kupata mtoto wa kike Stormi Webster ambaye alizaliwa mwezi Februari 2018. Wawili hao wameripotiwa kufikia mwisho wa mahusiano yao huku suala la uaminifu likichukua nafasi.

Msichana anyedaiwa kuchukua nafasi ya Kylie kwa Travis amefunguka na kukanusha kujihusisha na rappa huyo kwa kudai kama ishu hiyo inamuathiri na angependa watu waache kuiongelea kwa sababu inaharibu mfumo wa maisha yao ya kawaida.

 3,281 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey