Sambaza

Label Ya 2 Chainz T.R.U Kushirikiana Na Atlantic Records

Siku chache baada ya kutangaza kuthibitisha umiliki wa sehemu ya hisa na kuwa mmoja wa wamiliki wa A3C Festival, Mkali huyo mwenye asili ya Atlanta Marekani, ametangaza dili nyingine ambapo safari hii ni ushirikiano kati ya T.R.U ambayo ni Label yake na Atlantic Records.

2 Chainz amesema anafurahia ubia wake na Atlantic Records, ambapo amesema mipango yake mikubwa ni kuchukua nafasi ya kubadilisha maisha ya watu wengine na kuwafanya wawe mamilionea, Rappa huyo wa ‘Gang Up’ amesema anaichukulia Record label yake kama shule ndiyo maana inaitwa T.R.U kwa maana ya The Real University (Chuo Kikuu Cha Ukweli).

Atlantic Records imempa 2 Chainz fursa ya kushare malengo yake, amefanya muziki mwingi sana na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa hivyo ameamua kuangalia maisha ya baadae kwa kuungana na Atlantic ili kusaidia vijana wengine wanaotaka kuwa wanamuziki wa mfano wa kuigwa.

Uzinduzi wa ushirikiano kati ya T.R.U na Atlantic Records umekuja sambamba na ”Shoot it out” ambao ni wimbo wa wasanii wa Label hiyo kwa ushirikiano na 2 Chainz mwenyewe.

 2,714 total views,  6 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey