Nay Wa Mitego: Naogopa Wake Za Watu, Nikioa Mtu Asidili Na Mke Wangu
Imekuwa muda mrefu tangu ndoa kati ya muigizaji Shamsa Ford na Chidi Mapenzi ivunjike, Nay Wa Mitego ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Shamsa amepiga stori na Isri wa Global TV Online na kuzungumzia ishu hiyo ambayo anatajwa kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo.
Nay Wa Mitego amesema alikuwa anamuheshimu kama mke wa mtu wala hakumbuki kama aliwahi kuongea nae wakati Shamsa yupo kwenye ndoa yake.
“Kama kuna mtu anasema mimi nilichangia Shamsa kuachika ni stori tu, mimi naogopa wake za watu coz mimi sipendi kuka**wa, hivyo nikija kuoa sitapenda mtu aje kudili na mke wangu.” amesemea Nay Wa Mitego ambaye amethibitisha kuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye hakutaka kumtaja.
Angalia Full Interview Hapa:
8,742 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa