Wiki mbili zilizopita, muigizaji Terrence Howard alipewa heshima ya jina lake kuwa moja kati ya majina zaidi ya 2000 yanayoonekana kwenye mitaa ya Hollywood (Hollywood Walk Of Fame). Staa huyo wa Empire alipokea heshima hiyo siku chache baada ya kutangaza kuwa atastaafu kuigiza baada ya sirizi  yake na FOX kumalizika.Katika hali ambayo sio mashabiki wake tu bali hata wadau wa muvi hawakutegemea, mambo yameonekana kubadilika kwa muigizaji huyo ambaye ataonekana kwenye filamu mpya inayokwenda kwa jina la Triumph, stori ya mtoto wa kiume mwenye ndoto ya kuwa mwana mieleka.

Terrence Howard ni miongoni mwa mastaa ambao taarifa za kustaafu kazi zao zimewashtua mashabiki wao, staa mwingine ambaye ametangaza kustaafu ni Nicki Minaj lakini bado anaendelea kufanya kazi na wasanii wengine hivyo wawili hao wameonekana kuwadanganya mashabiki wao.