Sambaza

Celine Dion Na Stori Ya Mwanaume Mmoja Tangu Ana Miaka 12

Celine Dion alimpoteza mpenzi wa maisha yake imepita miaka minne sasa. Mashabiki wake wamekuwa wakitamanai kumuona akiwa na furaha kwa kutaka kumuona yupo kwenye mahusiano na mtu mpya. Hata hivyo, Dion hayupo tayari kufikia hatua hiyo. Kama utakumbuka tuliwahi kuandika kuhusu muimbaji huyo kusema ame-miss kuwa karibu na mpenzi wake na kuambiwa ni mrembo.

Celine Dion alikutana na mume wake Rene Angelil alipokuwa na umri wa miaka 12. Ilikuwa ni wakati ambao wawili hao walikuwa wakifanya kazi kama msanii na prodyuza wake. Baada ya Celine kufikisha miaka 19, walianzisha mahusiano na wakati huo mume wake alikuwa na miaka 45.

Mwaka 1994, wawili hao walifunga ndoa ambayo imekuwa ikitajwa miongoni mwa ndoa za mastaa zilizodumu muda mrefu, Celine Dion aliwahi kusema kama Angelil ni mwanaume pekee aliyewahi kuwa nae katika kipindi chote cha maisha yake.

Baada ya miaka 22 ya ndoa, mume wa Celine Dion alifariki kwa kansa ya koo akiwa na umri wa miaka 73 na kumuachia Celine Dion watoto wao watatu.

Celine Dion hataki kukutana na mtu yeyote mpya ambaye ataingia kwenye maisha yake,

Mwanzoni mwa mwaka huu, kulikuwa na tetesi kama mkali huyo wa ‘My Heart Will Go On”, alikuwa anatoka kimapenzi na densa wake anayeitwa Pepe. Lakini Celine alikanusha tetesi hizo kwa kusisitiza Pepe ni rafiki yake ambaye amekuwa akimsaidia Celine Dion kuchagua aina za uvaaji na kufanya mazoezi pamoja.

 2,877 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey