Lion Heart Ya Genevieve Nnanji Inawakilisha Nigeria Oscars 2020
Wakati anahangaikia kutafuta nafasi ya kuonyesha ubora wake, msichana mmoja anaikubali changamoto ya kushirikiana na Kaka yake wakati Baba yao ambaye ni Chief analazimika kuachia madaraka kutokana na matatizo ya afya. Ni hadithi inayoonekana kwenye filamu ‘Lion Heart’ ya muigizaji Genevieve Nnanji wa Nigeria ambayo imepata shavu la kuwania tuzo za Oscars mwaka 2020.
Kamati ya filamu Nigeria imeichagua filamu hii kama filamu itakayowakirisha Nigeria kwenye tuzo hizo zitakazotolewa Februari 9,2020.
Filamu hiyo iliandaliwa na kuonekana kwa mara ya kwanza nchini Nigeria December 19 na kuachiwa duniani kote January 4,2019. Lion Heart ni filamu ya kwanza iliyotengenezwa ndani ya Nigeria kununuliwa na kuonekana Netflix.
Mbali na Genevieve Nnaji,, Filamu hii ina mastaa kama Pete Edochie,Nkem Owoh, Onyeka Onwenu, Kanayo .O. Kanayo, Chika Okpala, Kalu Ikeagwu, Sanni Mu’azu, Yakubu Mohammed, Ngozi Ezeonu, Peter Okoye (P-Square), na Chibuzor Azubuike (Phyno).