Uchaguzi Serikali Za MitaaRais Magufuli Awataka Wananchi Kujiandikisha
Serikali imewataka wananchi wote nchini kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba, 24 mwaka huu.
Akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga eneo la Naila Halmashauri ya Sumbawanga hapo jana, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewaasa watanzania wote kuitumia haki yao ya msingi katika kuendeleza demokrasia nchini kwa kuchagua Viongozi bora wanaojali shida za wananchi waishio katika majijij, miji, vijiji, mitaa na vitongoji ambapo viongozi hao huwajibika kwa wananchi waliowachagua na kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani Rukwa ambapo anatarajiwa kuhitimisha ziara yake mkoani humo kwa kufungua hospitali mpya ya Wilaya ya Nkasi pamoja na kituo cha afya Namanyere pia kipo wilayani Nkasi kabla ya kuanza ziara yake mkoani Katavi.
2,643 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa