Sambaza

Mke Wa T.I Ameibiwa Vitu Vya Bilioni 1.7

Tameka ”Tiny” Harris, ambaye ni staa wa TV, muimbaji na mke wa Rappa T.I, alikuwa na samani zinazogharimu bilioni 1,72 zilizoibiwa wikiendi iliyopita. Pete ya ndoa, saa na heleni  ni vitu ambavyo mwanamke huyo ameibiwa ndani ya gari yake.

Mke wa T.I aliwaambia polisi kuwa, wizi huo ulitokea wakati yeye na rafiki yake walipokuwa wakipata kinywaji kwenye Baa moja mjini Atlanta, ambapo alirudi kwenye gari yake na kukuta vitu hivyo havipo.

Polisi wamedai hapakuwa na ishara yeyote ya gari ya mwanamma huyo kuvunjwa, lakini Tameka alisisitiza kupotelewa na begi iliyokuwa na vitu hivyo akiwa maeneo hayo

Upelelezi wa kumgundua mwizi unaendelea wakati ambao Tiny amegoma kuongea na mapaparazi juu ya ishu hiyo ambayo imeonekana kukosa ushahidi.

 3,684 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey