Sambaza

Albamu Ya Kanye West Imevuja

Mashabiki wa Kanye West walikuwa wanategemea kupata muziki mpya kutokea kwa Rappa huyo ambaye aliahidi kuiachia albamu yake yenye nyimbo za dini, Jesus Is King ilipangwa kuachiwa Septemba 27 na baadae ikatangazwa haijakamilika hivyo itaachiwa mwaka 2020.


Wiki iliyopita kupitia YouTube ulivuja wimbo wa Kanye West ambao haukuwa unasikika vizuri kutokana na kelele zilizokuwa zikisikika na ubora wa kurekodiwa ulikuwa wa kiwango cha chini sana. Katika hali isiyo ya kawaida, Siku ya jana Kanye West ameendelea kuwa tageti ya nyimbo zinazovuja mara baada ya albamu iliyopewa jina ‘Kanye Drop Your Albums’ kupakiwa kwenye Spotify na Tidal zikiwemo kolabo na Justin Bieber, Post Malone,Dolla $ign, XXXTentcion, Nicki Minaj, Young Thug, Chance the Rapper, Travis Scott na A$AP Rocky.

Hatuna uhakika kama nyimbo hizi zinaweza kuwa na uhusiano na Jesus Is King. Tunachofahamu albamu hiyo bado haijakamilika

 

 1,739 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey