Sambaza

Kendall Jenner Ni Mjamzito?

Kwenye episode iliyopita ya Keeping Up With The Kardashian, Kendall Jenner alimwambia Kim Kardashian kama hawezi kusubiri kuitwa mama, mashabiki wa mrembo huyo wamekuwa wakijadili kauli hiyo ambayo imekuwa ikiwapa utata.

Kauli ya mwanamitindo huyo ambaye ni dada wa Kylie Jenner, imewafanya mashabiki wake kufikiria huenda akawa amenasa ujauzito na hizi zikawa ni taarifa rasmi za mrembo huyo kutarajia kuitwa mama muda si mrefu.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na Kendall, mwanamitindo huyo hana presha ya kuwa na mtoto kwani bado ana mambo mengi ya kufanya na kazi yake ya fasheni. Aliposema hawezi kusubiri kuwa mama alimaanisha huo ni mpango wake wa baadae kwanI Kendall bado anajiona msichana mdogo sana.

Kendall Jenner ni mtoto wa nne kati ya wasichana watano amabao wote ni watoto wa mwanamama Kris Jenner, Kendall ndiye memba wa familia hiyo ambaye amebaki hana mtoto. Mdogo wake Kylie Jenner ana mtoto wa kike ambaye amezaa na Rappa Travis Scott waliyeripotiwa kuachana mwishoni mwa mwezi uliopita.

 

 4,380 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey