Kukosekana Nishati Mbadala Ni Chanzo Cha Michepuko
Kukosekana kwa nishati mbadala (jadilifu) kumeweza kupelekea ongezeko la michepuko kwenye jamii.
Akiongea kwenye kipindi cha Mid Morning Fresh kinachoruka +255 Global Radio, Afisa habari wa TGNP Bi. Neema Mwinyi amesema kuwa kukosekana kwa nishati mbadala kumechangia ongezeko la michepuko na mivurugano kwenye baadhi ya familia.
Bi. Neema ameyasema hayo alipokuwa akichangia maada iliyohoji jinsi ambavyo nishati mbadala inaweza kupunguza ukatili wa kijinsia majumbani. Afisa huyo ametaja changamoto nyingi wanazokutana nazo wanawake ikiwemo kupigwa na waume zao kwa kutumia muda mwingi wanapokuwenda kutafuta kuni.
Bi. Neema amesema ni muhimu kwa jamii kutumia nishati jadilifu kama gesi asili(Baiyogasi) pamoja na makaa ya mawe ili iweze kuwa rafiki na mazingira