Sambaza

Bonge La Nyau; Alikiba, Kufanya Kazi Na Wasafi, Ugomvi Na Bob Junior

Bonge La Nyau ameitaja sababu ya kuacha kurekodi na Bob Junior.

Stori zilizokuwepo mjini ni ugomvi kati ya Bonge La Nyau na Prodyuza wake Bob Junior,  kilichokuwa kinasemekana, kuna ugomvi mkubwa uliosababisha wawili hao kushindwa kufanya kazi tena. Bonge La Nyau leo amezipiga chini tetesi hizo ambapo amedai kuwa yeye na Bob Junior ni familia moja.

“Unajua kuna kipindi studio ilisimama kufanya kazi, kwa hiyo mimi nisingejiongeza kwenda kurekodi sehemu nyingine ina maana na mimi mwenyewe ningesimama muziki wangu, kwa hiyo mimi pale nikajiongeza nikamtafuta Amiga nikahamia studio zake za kariakoo ndio ukaribu na Bob Junior ukaanza kupungua. amesema Bonge La Nyau alipokuwa akijibu swali la Stewart George aliyetaka kujua ukweli wa ishu hiyo.

Bonge La Nyau amethibitisha kama hakuna ugomvi kati yake na Bob Junior. Kwenye kauli nyingine Bonge La Nyau amesema ukaribu wake na Alikiba na Bob Junior ambao wote ni wapinzani wa Diamond Platnumz haumfanyi ashindwe kufanya kazi na msanii huyo au timu yake ya Wasafi. “Watu wanashindwa kuelea vitu, mimi na Alikiba tumekua pamoja na Bob Junior, Diamond hakuwa rafiki yangu kipindi hicho tumejuana kupitia Sharobaro Record”, kuhusu kufanya kazi na wasanii au matamasha ya wasafi, Bonge La Nyau amesema inawezekana, amekiri kama ukimya wake ulichangia yeye kukosa nafasi, Nyaulosa amesema anadhani kama akitoa kazi nzuri atajumuishwa kwenye movements zote watu wategemee mambo mazuri”.

Bonge La Nyau ameyasema hayo kwenye kipindi cha Bongo255 kinachoruka +255 Global Radio, Jumatatu mpaka Ijumaa, Rashid Mbegani ni mtangazaji mwenza wa kipindi hicho ambaye alimuuliza Bonge La Nyau kuhusu mtindo wa Alikiba kukaa muda mrefu bila kuachia wimbo, ”Alikiba ana mitazamo fulani ambayo usipomjua unaeza ukam-doubt, Ali amejitengenezea mazingira ya kufanya ngoma moja ikaishi muda mrefu, kwa upande wake yeye anahisi ni sawa, lakini kwa kile ambacho mashabiki wanakitaka inakuwa sio sawa, inabidi kusikiliza watu wanataka nini… hakuna mtu anapinga uwezo wake juzi nimekutana nae amenisikilizisha ngoma zake na video mpya, nadhani kabla mwezi haujaisha atafanya kitu kikubwa” alijibu Bonge La Nyau.

Bonge La Nyau amerudi kwenye muziki baada ya ukimya wake na Kitochi aliyoifanya na Barnaba ndio bidhaa yake mpya mjini.

Unaweza Kuicheki video yake hapa.

 6,301 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey