Harmonize Ametangaza Menejimenti Yake Na Wimbo Mpya
Imekuwa muda mrefu sasa tangu battle kati ya Harmonize na WCB Wasafi, Mambo yanaonekana kuwa bab kubwa kwa mmakonde huyo ambaye anazidi kuonyesha maajabu yake kila kukicha.
Harmonize amekuwa akitengeneza umaarufu wa Konde Gang ambayo aliwahi kuitaja kama sio Record Label bali ni familia ya watu wanaoshirikiana kusogea. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alhamisi(Oktoba 10) Harmonize ameitangaza Konde Music Worldwide kama menejimenti yake mpya.
Sambamba na utambulisho wa KMW, Harmonize alipokuwa aki-reply kwenye moja ya comment ametangaza wimbo mpya utakaotoka wiki ijayo.
3,504 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa