Meek Mill; Nimeyachoka Mapenzi, Bora Kuwachezea Wanawake.
Mapenzi ni kitu ambacho kila mmoja anakifurahia wakati ambao anakuwa na nyakati nzuri na yule ampendaye, Mapenzi hayo huonekana miyeyusho pale ambapo wawili wanaopendana wakitofautiana hata kuiruhusu chuki kuingia kati yao. Meek Mill ni miongoni mwa wanaopitia mazingira magumu kwenye kipengele cha mapenzi.
Tangu alipoachana na Nicki Minaj, Rappa huyo ameyaweka mahusiano yake mbali na media, inasemekana Meek anasumbuliwa sana na mapenzi pamoja na mtindo wa maisha yake ikiwemo uhuru wake.
Meek Mill ameamua kuziweka wazi hisia zake kwa kusema mapenzi yamemchosha, hivyo anaona ni bora kuwatumia wanawake, Kupitia ukurasa wake wa twitter, Mkali huyo wa ngoma ya ”All Eyez On Me” ameelezea anavyojisikia kama unavyoweza kusoma hapa chini.
Love is getting scary that’s why I’m just tryna f#%k
— Meek Mill (@MeekMill) October 5, 2019
And I just bought that rolls truck to take the pain away ?
— Meek Mill (@MeekMill) October 5, 2019