Gnako Anakuambia #TwenzetuMnadani
Msanii wa hip hop ambaye pia ni memba wa kundi la Weusi, Gnako warawara ameanzisha mnada utakaowapa fursa ya kuwakutanisha wakulima, wafanyabiashara pamoja na wanunuzi.
Kwenye kipindi cha Mid Morning Fresh kinachoruka +255GlobalRadio, Leo Gnako amesema lengo la kuanzisha projekti hiyo ni kuwasaidia wanunuzi kupata vitu vyote kwa wakati mmoja, lakini pia kuwasaidia wafanya biashara wote kuonesha bidhaa zao na kuuza kwa urahisi.
Mnada huo utakoitwa Twenzetu mnadani ni, utahusisha bidhaa zote ikiwemo vifaa vya nyumbani, nguo, vyakula, na vitu vingine vingi ikiwemo michezo ya watoto na burudani mbalimbali watakazopata watu ambao watatembelea Mnada huo.
2,428 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa