Sambaza

Gnako: Harmonize Na Diamond,Kolabo Na Maua Sama

Leo asubuhi kwenye kipindi cha Mid Morning Fresh, Gnako ameitambulisha Gusanisha ambayo ni ngoma yake mpya na Maua Sama.

Akipiga stori na Diana Mkeu, Babu Ally na Dar Boi ambao ni watangazaji wa kipindi hicho, Gnako amesema yeye na Maua Sama ni marafiki ambao wamefanya kazi nyingine pamoja. “Mimi na Maua Sama ni washikaji ambao tumeshafanya kazi nyingine… siku moja alinikuta studio nafanya kazi zangu nyingine ikatokea hii beat (gusanisha) nikawa nafanyia kitu ambacho sikua na uhakika nacho, Maua alipotokea akanishawishi kwa kuniomba achangie kitu baada ya kuona vibe ya watu wa karibu yangu ikanibidi kuiachia ngoma hii japo sikuwa tayari kuiachia kwa muda huu. amesema Gnako.

The A-City Finest pia amejibu kuhusu kufanya kazi na wawili kati ya Diamond Platnumz na Harmonize, Gnako amesema Kolabo ni koneksheni, kama hakuna koneksheni nzuri hakuna kolabo itakayofanya vizuri. Hivyo ni lazima pawe na muunganiko mzuri kati ya wasanii wanaokutana kufanya kolabo.

Gnako Warawara ambaye anatamba na ngoma ya Gusanisha, amewapa ushauri wasanii wachanga kwa kuwaambia wanatakiwa kuja na vitu tofauti ambavyo wasanii waliotangulia hawajavifanya huku akiwataka vijana kuacha kulalamika badala yake watumie muda huo kutafuta fursa.

 

 3,624 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey