Sambaza

Tyga Ameshambuliwa Na Mashabiki Kisa Viatu Vya Travis Scott

Watu Wanaojiita ni mashabiki wa Rappa Tyga wameonyesha kukerwa na kitendo cha mwanamuziki huyo kuvaa viatu vya Travis Scott.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mkali huyo wa ngoma ya Taste amepost picha akiwa kwenye ferrari yake nyekundu huku miguuni amevalia viatu vya JordanxTravis Scott ambavyo vimeonekana kutrend siku za hivi karibuni.
Mashabiki hao wamekiita kitendo hicho na kujidhalilisha kwani Travis Scott ni mtu ambaye alimpokonya Tyga mrembo wake Kylie Jenner.
Picha hii ya Tyga kuvaa viatu hivyo imekuja siku chache baada ya taarifa za kuachana kwa Travis Scott na Kylie ambao walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Stormi Webster.

 4,518 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey