Sambaza

Rais Magufuli Amewatatetea Viboko Katavi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo oktoba 12 amemaliza ziara yake mkoani Katavi ambapo amekuwa akiwahutubia wananchi na kufungua miradi mbalimbali ikiwemo safari ya ndege ya ATCL Dar- Mpanda.

Akiwahutubia wakazi wa mkoa huo, Jana Rais Magufuli aliagiza Mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA) kuwanusuru viboko waliokuwa wamekosa maji kwenye bwawa lao na kuanza kuingia mitaani kutafuta maji.

Rais Magufuli aliwataka wahifadhi wa Bwawa hilo kuhakikisha wanawawekea maji wanyama hao ili waendelee kufurahia maisha yao kwa sababu asili yao ni kwenye maji.

Baada ya agizo la Rais Magufuli, watu wa TANAPA waliweza kufika kwenye bwawa hilo na kuwawekea maji viboko hao kama unavyoweza kuona hapa.

 2,558 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey