Sambaza

Picha; Mtu Anayedhaniwa TUPAC Ameonekana Afrika Kusini

Septemba 13 mwaka huu, Imetimia miaka 23 tangu kilivyoripotiwa kifo cha 2 Pac ambaye ameendelea kuishi kwenye mioyo ya mashabiki wengi wa Hip Hop.


Tupac ameendelea kutajwa miaka yote ya kutokuwepo kwake kutokana na mambo mengi aliyoyafanya katika umri wake mdogo, lakini kitu cha ajabu zaidi ambacho husemwa na kutengeneza mitazamo tofauti ni kuhusu utata wa kifo cha rapper huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 25.
Inasemekana 2 PAC na timu yake walidanganya kuhusu kifo chake siku 6 baada ya watu wasiojulikana kumpiga risasi akiwa kwenye gari yake barabarani. Taarifa za kuonekana staa huyo wa Dear Mama, hazijasikika mara chache, wapo ambao wamekuwa wakisema wamemuona au kusikia taarifa zake kuwa anaishi.
Kwa mara nyingine, mtu anayedhaniwa kuwa ni Tupac ameonekana Afrika Kusini. Kwenye picha iliyopigwa gizani, anaonekana mwanaume mtu mzima kwenye umri kati ya miaka 40 na kitu huku sura yake ikifananishwa na Tupac.

 4,111 total views,  9 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey