Sambaza

Wizkid; Sifanyi Muziki Ili Niwe Staa Wa Afrika

Mwanamuziki kutokea Nigeria ambaye anafanya vizuri Kimataifa, Wizkid amesema kuwa wakati anaanza kufanya muziki hakufikiria kuwa supastaa wa Afrika.

Wizkid amesema alitamani kufanya muziki ambao ungesikilizwa Duniani kote. Kwa mujibu wa WizKid, Muziki ni lugha ambayo watu wote wanaweza kuielewa hivyo hakuna mtu ambaye anaweza kuisikiliza aina ya muziki wake halafu akaacha kufurahia, labda kama mtu huyo atakuwa hapendi muziki kitu ambacho hakiwezekani (kila mmoja anapenda muziki).

Wizkid ameyasema hayo kwenye intavyuu na Gazeti moja la Uingereza ambapo amesema kitendo cha kufanya shoo moja na Beyonce ni sehemu ya mafanikio ya muziki wake, huku akikifananisha kitendo cha kuhusika kwenye Albamu ya ‘Lion King’ kama dili kubwa miongoni mwa alizowahi kupata.

Wizkid kwa sasa anatamba na wimbo JORO aliouachia Septemba 30 mwaka huu. Unaweza kuicheki Video yake hapa.

 3,400 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey