Harmonize Amethibitisha Kolabo Na WizKid
East African Young King, Harmonize yupo Melbourne Australia alipokwenda Kwenye shoo ya One Dance Afrika.
Kwenye shoo hiyo, Kondeboy amepata nafasi ya kuperfom na Mama Afrika Yemi Alade alongside starboy Wizkid ambao amekuwa akiroll nao hata baada ya shoo.
Jana (Oktoba 12), Harmonize alishea moments zake na Yemi Alade, siku ya leo ametupia picha zake na Wizkid huku caption yake akiwa ameandika kitu kinachoashiria kuna kolabo kati yake na staa huyo wa Nigeria.
Mwanzoni mwa wiki hii Harmonize aliitambulisha Konde Music Worldwide kama menejimenti yake mpya, na kwenye moja ya komenti ambazo Harmonize alijibu, ilikuwa ni kuthibitisha ujio wa ngoma mpya wiki ijayo.
Mashabiki wamekuwa excited kuona Wizkid anafanya kolabo yake na Mtanzania kwa mara ya kwanza.
Nini unafikiri unaweza kuwa mtazamo wako?
6,508 total views, 3 views today