Binti Yake Chris Brown Amvutia Justin Bieber
Chris Brown aliwahi kumuita mtoto wake pacha wake kwenye caption ya picha yao ya pamoja walipokuwa wakiangalia moja kati ya video za ngoma zake.
Umefika wakati wa kuelewa kwanini Breezy alisema wao ni mapacha.
Oktoba 10 Chris alipost video ikimuonyesha mtoto Royalty akiicheza kwa mbwembwe ngoma ”Gimme That,” Michezo ya mtoto Royalty kwenye video hii inaonyesha jinsi alivyo makini na ni kiasi gani anapenda kucheza muziki.
Licha ya kuwa hakucheza vizuri sana, lakini kuna chembechembe za Baba yake zinazoonekana kwenye moves zake, kama ambavyo tunafahamu ukali wa Chris Brown kwenye kucheza muziki.
Justin Bieber ni miongoni mwa waliovutiwa na uchezaji wa Royalty hata kuweza kutoa muda wake na kuandika maoni yake juu ya mtoto huyo ambapo alimsifia kuwa ni mwenye kipaji.
Bila shaka nyota ya mtoto huyu imeanza kung’aa mapema na dunia itegemee kuona legacy ya Chris Brown ikiendelea kuishi kupitia binti huyu ambaye kwa sasa ana umri wa miaka mitano.
2,604 total views, 3 views today