Eddy Kenzo Atishia Kuacha Muziki
Zaidi ya mwezi mmoja umepita tangu Eddy Kenzo alipoanza kupitia kipindi kigumu kwenye maisha yake ya mapenzi,
Kwa mujibu wa watu wa karibu yake, Eddy Kenzo amekuwa mkimya na imara kwa wakati mmoja na hii ni kutokana na mpenzi wake anayetambulika kwa jina la Rema kuolewa na mwanaume mwingine.
Eddy Kenzo anadaiwa kuwa bado ana mapenzi ya kweli na Rema hata kama yeye anampenda mwanaume mwingine.
Hakuna kitu ambacho kinaweza kuzuia mipango ya Rema na mumewe Sebunya kuendelea na mipango yao, kwenye maelezo ambayo Sheikh Nu Muzaata wa Uganda alitoa, yanamtafsri Eddy Kenzo kama mwanaume ambaye hajatulia, Baada ya kuzipata stori hizo, Eddy Kenzo ameielekeza hasira yake yote kwa Sheikh huyo akimtaka atengue kauli yake vinginevyo mshindi huyo wa tuzo ya BET ataacha kufanya kazi ya muziki kwenye steji yoyote nchini Uganda.
2,984 total views, 3 views today