Kanye West Amethibitisha Kuhamia Kwenye Ukristo Na Tarehe Ya Kuachiwa Jesus Is King
Wakati umati wa watu ukifurahishwa na tangazo la Kanye West wakati wa kusikiliza albamu yake katika Chuo Kikuu cha George Washington Lisner Washington D.C. Jumamosi, kwamba Jesus Is King imepangwa kutolewa Oktoba 25, uthibitisho mwingine wa kuwaaminisha watu ulitokea.
Kanye alithibitisha kwamba hivi karibuni alibadilisha dini na kuhamia kwenye Ukristo.
“Nataka kukujulisha kuwa mimi sipo hapa kwa ajili ya burudani yako alasiri hii,Tuko hapa kueneza injili”. Kanye West aliambia umati wa watu. “Mnisamehe ikiwa nitawapuuza kwa kitu chochote,” aliongeza. “Mimi nnimebadilisha dini hivi karibuni. Inamaanisha kuwa nimeokoka mwaka huu.”
Mchungaji wa Kanye, Adam Tyson, aligusia mwelekeo huu mpya wa Kanye kwa kuwataka watu wamuamini Kanye, wala wasionyeshe haja ya kuwa na wasiwasi naye kwani ameokoka kweli.
1,923 total views, 3 views today