Marioo Na Dogo Janja Kwenye Wimbo Wa Pamoja
Tamasha la muziki la Fiesta bado linazunguka kwenye baadhi ya miji ya Tanzania iliyochaguliwa kupata bururdani hiyo ambapo wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakiwapagawisha mashabiki wao.
Marioo ni miongoni mwa wanamuziki waliopata nafasi ya kukutana na mashabiki wao na kuwapa burudani ya nguvu kupitia jukwaa la fiesta mwaka huu.
Kwenye picha ya pamoja na Dogo Janja, Marioo ametangaza ujio wa ngoma ya wawili hao ambayo hatuna uhakika kama ipo tayari au Marioo amejaribu kuchukua attention yetu. Kwenye caption ya picha hiyo, Marioo ameandika “Goma letu sijui tulitoe lini ? @dogojanjatz #wakakawenyeFuture“. Dogo Janja amereply kwenye post hiyo kwa kuandika #KIADUI ambayo tunahisi inaweza kuwa title ya ngoma yao.
Hii itakuwa kolabo ya kwanza kuwakutanisha wawili hao ambao ni miongoni mwa wanamuziki wa Bongofleva wenye umri mdogo wanaokubalika na mashabiki wa muziki.
6,560 total views, 3 views today