Highest In The Room, Travis Scott Ameingia Nafasi Ya Kwanza Billboard Hot 100
Moja kati ya stori zenye mashabiki wengi kuhusu Travis Scott, ni ishu ya kupigana chini na Kylie Jenner ambaye ni Mama wa mtoto wake wa kike anayeitwa Stormi Webster.
Mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu wawili hao ambao mwishoni mwa wiki iliyopita, waliripotiwa kuwa na mazungumzo ya kurudiana ili waendelee kumlea mtoto wao. Licha ya kuwa macho na masikio ya wengi yapo kwao, hiyo hiwazuii kufanya vitu vingine, Travis Scott ana ngoma mpya inayoitwa ‘Highest In The Room’ wimbo ambao inasemekana ameufanya kuelezea mahusiano yake na Kylie.
Baada ya wiki moja kupita tangu iachiwe, ngoma hiyo imefanikiwa kuingia nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard Hot 100, ikiwa ni ngoma yake ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka huu.
Video ya wimbo huo ambayo iliachiwa usiku wa Oktoba , inamuonyesha Travis Scott kama mtu anayejitetea kwa kupamabana licha ya mateso anayokutana nayo lakini mwisho anashinda.
Ikiwa na siku 13 YouTube, Video hiyo ambayo imekuwa directed na Travis Scott na Dave Mayers imetazamwa zaidi ya mara milioni 37.
Hii inakuwa ngoma yake ya pili kushika nafasi za juu katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita baada ya SICO MODE aliyoifanya na Drake kushika nafasi ya pili kwenye chati hiyo mwishoni mwa mwaka 2018.
3,986 total views, 3 views today