Rais Magufuli Ametangaza Mabadiliko Jimboni Kwa Nape
Rais Magufuli ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuitwa Halmashauri ya Mtama na Makao Mkuu ya Halmashauri hiyo yahamishiwe Mtama kutoka Mjini.
Amesema, ndani ya siku 15, Viongozi wa Halmashauri hiyo watoke Mjini na kuhamia Mtama na hiyo ndio italeta maendeleo kwani kama ni giza ndio watashughulikia umeme haraka.
Aidha, amesema “Najua kulikuwa na mabishano, wapo wanaotaka Makao Makuu yaende Subi, wapo waliotaka yaende Mchinga, wapo waliotaka yaende Rondo, kila mmoja alitaka.” Amefafanua, “Kwa kuwa mimi ndio Rais, na mimi napasua katikati kwa kufuata haki, nimetoa maagizo, Manispaa ya Lindi itachukua eneo lake iliyokuwa nalo mpaka Mnazi Mmoja hadi Mingoyo na kuongezewa eneo la Mchinga.
2,315 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa