Salaam Za Harmonize Kwa Rais Magufuli, Tanzania Na Serikali Yake
Jana Oktoba 14, ilikuwa kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki Uingereza mwaka 1999.
Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere imeambatana na kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru ambao umezimwa rasmi mkoani Lindi zilikofanyika sherehe hizo. Harmonize ambaye asili yake ni Mtwara, alikuwa jirani na nyumbani kwao kuwaburudisha wakazi wa eneo hilo akitokea nchini Australia alipokwenda kwenye shoo ya One Dance Africa.
Baada ya kupeform wimbo wa Magufuli, Viongozi wa nchi akiwemo Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walinyanyuka na kuungana na Harmonize kuucheza muziki huku wakimtunza msanii huyo vibunda vya maana.
Harmonize ametumia Instagram kuelezea mapenzi yake kwa Tanzania na viongozi wake ambapo amemtaja Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kama mtu aliyemshawishi kuwepo hapo kwa mualiko maalum wakati ambao msanii huyo hakuwepo Tanzania.
“I don’t play around when it’s come to my beautiful country Tanzania…!!!! I was there 2 represent all ?? Youth thanks again Mr President Doctor John Pombe Magufuli my number one supporter I’m grateful ?? lakini pia kipekee kabisa nimshukuru mheshimiwa P.M. Kassim Majaliwa Kassim kwakunipa molari na msisitizo nisipitwe na hili tukio ukizingatia sikuwa nchini Ila kwa uzito wa kauli yako na kuthamini uwepo wa Serikali yangu pendwa nilifanikiwa kuwahi …!!! bila kusahau mama yangu makamu wa Rais Mama Samia Suluhu nakushukuru sana Na ile bahasha imefanya siku yangu ikawa ya kipeke mno…!!! Pia shukrani za kipekee zikuende waziri mwenye dhamana Ya michezo sanaa burudani baba yetu Docter Harison Mwakyembe shukrani baba…!!!!! viongozi wote wa serikali mliosimama kwa ishara ya upendo na kupendezwa kile anachokifanya kijana wenu…!!! Mungu awabariki Sana….!!!! ????….. #HappyBabaWaTaifaDay
#HappyKileleChaUkimbizajiWaMwengeWaUhuru @Kondegang“
Harmonize ambaye ameendelea kung’aa kwenye sherehe mbalimbali za kiserikali tangu alipoachia wimbo wa ‘magufuli’ unaopata mashavu maeneo mengi anapokuwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli ambaye Harmonize anamtaja kama mtu namba moja anayemuunga mkono.
6,158 total views, 3 views today